Rais
Mstaafu wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amewasilisha ujumbe maalumu kutoka kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenda
kwa Rais wa Jamhuri ya Senegal, Mhe. Bassirou Diomaye Faye jijini Dakar.
Katika
mazungumzo yao ya kirafiki, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete alieleza dhamira ya dhati ya
Rais Dkt. Samia na Serikali anayoiongoza ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa
kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Senegal.
Pamoja na
masuala ya ushirikiano wa kiserikali, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa
kukuza uhusiano baina ya wananchi wa mataifa haya mawili kupitia sekta za
elimu, biashara, utalii, na maendeleo ya vijana na wanawake.
Ziara hii ni
sehemu ya juhudi endelevu za Tanzania kuimarisha uhusiano wa kimataifa na
mataifa ya Afrika Magharibi, huku ikiweka msisitizo kwa diplomasia ya uchumi na
ushirikiano wa watu kwa watu.




0 Maoni