Bodi ya Wadhamini TANAPA yahitimisha kikao cha 209

 

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jenerali (Mstaafu) George Waitara imehitimisha kikao cha 209 jana Machi 14, 2025 kilicholenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo ya Shirika.

Kikao hicho kilitanguliwa na vikao vya kamati mbalimbali ambazo ni Kamati ya Ukaguzi na Utawala Bora inayoongozwa na CPA Hadija Mohamed Ramadhani, Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Kamati ya Himasheria na Usimamizi wa Hifadhi inayoongozwa na Dkt. Robert Fyumagwa, Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa kamati hiyo, pamoja na kikao cha Kamati ya Utalii na Huduma za Shirika kilichoongozwa na Dkt. Rhimo Nyansaho, Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, Bodi ilifanya ukaguzi wa  miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Banagi - Lobo - lango la Kleins yenye urefu wa kilomita 72, barabara ya Golini - Naabi - Seronera yenye urefu wa kilomita 68 na ujenzi wa uwanja wa Golf “Serengeti National Park Golf Course”inayotekelezwa na kampuni tanzu ya TANAPA “TANAPA Investment Limited (TIL)” na ujenzi wa lango la Kleins unaotekelezwa na kampuni ya Stance Technic and Civil Engineers Limited.



Chapisha Maoni

0 Maoni