Watumishi wa Umma warejea Dar kutekeleza haki yao ya kupiga kura

 

Baadhi ya watumishi wa umma ambao vituo vyao vya kupigia kura vipo katika Jiji la Dar es Salaam wamewasili jijini humo kwa ajili ya kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Wamesema kuwa zoezi linaendelea kwa utulivu na usalama mkubwa, huku wakieleza kuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha kila mwananchi anapata nafasi ya kushiriki kikamilifu.

Miongoni mwa watumishi hao ni Afisa Habari kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Sixmund Rugashe, ambaye ametokea Dodoma na kuja kupiga kura katika kituo cha Bunge kilichopo Manispaa ya Ilala. Begashe amesema amefurahishwa na jinsi wananchi wanavyojitokeza kwa wingi, hali inayoonesha dhamira ya kweli ya Watanzania kushiriki katika kuamua mustakabali wa Taifa lao.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania wote waliopo nchini kuhakikisha wanajitokeza kwa amani na utulivu katika vituo vyao vya kupigia kura, ili kuchagua viongozi wanaowaamini na wanaowataka kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi, akibainisha kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya Taifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni