Jaji Mkuu Mhe. Masaju ashiriki zoezi la upigaji kura Dodoma

 

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 29 Oktoba, 2025 ameungana na Watanzania wengine nchini kutimiza haki yake ya Kikatiba kwa kushiriki katika zoezi la upigaji kura wa Rais, Wabunge na Madiwani katika Kituo cha kupigia Kura cha Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma.

Mhe. Masaju aliwasili katika viwanja vya Kituo hicho majira ya Saa 2 Asubuhi na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambaye pia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akiwa katika zoezi la upigaji kura leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akipakwa wino maalum kama ishara ya kumaliza zoezi la upigaji kura leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma.

Chapisha Maoni

0 Maoni