Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Philip Mpango amejitokeza kupiga kura akiwa miongoni mwa wananchi wa Kijiji cha
Kasumo wilayani Buhigwe mkoa wa Kigoma, walishiriki zoezi hilo.
Dkt. Mpango amepiga kura ya kuchagua Rais, Mbunge na Diwani leo Oktoba 29, 2025, ambapo Watanzania kwenye maeneo mbalimbali nchini wanashiriki kuchagua viongozi watakaolingoza Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kwa ujumla hadi sasa zoezi la upigaji kura katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar linaendelea kwa amani na utulivu, huku wananchi wakijitokeza kutekeleza wajibu wao wa Kikatiba wa kuwachagua viongozi wao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Kariakoo, Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini Unguja.
Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye akifurahi kwa kuonyesha kidole chake baada ya kupiga kura leo.





0 Maoni