Samia Infastructure Bond hati fungani Mahususi inayotolewa
na Benki ya CRDB, kwa ajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini
Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
(TARURA), leo imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), hatua
hiyo imejiri baada ya kukusanywa kiasi cha bilioni 323 kutoka Taasisi
mbalimbali na wawekezaji binafsi.
Zoezi hilo limeongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kupiga
kengele ikiwa ni ishara ya kuorodhesha Samia Infastructure Bond kwenye Soko la
Hisa la Dar es Salaam.
Samia Infastructure Bond inatazamiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya malipo ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara hivyo kuharakisha maendeleo ya miundombinu muhimu kwa usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma na bidhaa.
0 Maoni