Mwenyekiti TEF awataka waandishi kusoma Ilani za vyama vya siasa

 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari kusoma ilani za vyama vya siasa ili wawe katika nafasi nzuri ya kuhoji.

“Tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tusome ilani za vyama vya siasa vyote, turipoti habari zote na kusiwe na upendeleo wa chama chochote. Tujiandae kama wanahabari,” amesema.

Balile ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Februari 2025 jijini Dar es Salaam kwenye kikao kilichoandaliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni