Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Ndugu Kassim Majaliwa amesema
kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni tiba ya maendeleo hivyo watanzania
wanapaswa kwenda nae kwani ataifikisha nchi kule kunakotarajiwa.
Amesema kuwa
Rais Dkt. Samia ni kiongozi anayeona, kusikiliza na kutatua changamoto za
Watanzania kwa ustadi wa hali ya juu na amedhihirisha hilo katika kipindi chake
cha uongozi.
Ametoa kauli
hiyo leo Jumapili (Februari 16, 2025) wakati Mkutano Mkuu Maalum Chama cha
Mapinduzi Jimbo la Maswa Mashariki, uliofanyika katika uwanja wa nguzo
nane,Maswa mkoani Simiyu.
“Rais Dkt. Samia kwa uwezo wake na maono yake
ameonesha anadhamira ya dhati ya kuwatumikia watanzania, wote tumeshuhudia nia
yake ya kusimamia utekelezaji wa miradi katika sekta mbalimbali za maendeleo na
tumeona namna alivyosimamia kukamilisha miradi yote ya kimkakati,”
Akizungumzia
Sekta ya Maji Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi
imedhamiria kuhakikisha inatekeleza miradi mikubwa ya maji kutoka katika Maziwa
ya Victoria, Tanganyika na Nyasa lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na
upatikanaji wa maji safi na Salama “Mpango wetu ni kuendelea kufikisha huduma
ya maji mpaka vitongojini.”
Kadhalika,
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa katika sekta ya afya Serikali imeendelea kutoa
fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha huduma za afya zinaimarishwa na
kuwapunguzia adha wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Ameongeza
kuwa ili kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa Umeme inaimarika nchini, Serikali
imeendelea kutekeleza miradi umeme “Tumeshafikisha umeme karibu asilimia 99
kwenye vijiji vyetu, sasa tunakwenda vitongojini.”
Katika hatua
nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa chama hicho kipo imara na kinaendelea
kuwahudumia Watanzania.
Amesema kuwa
kutokana na sera imara zinazotekelezaka za chama hicho, kimeendelea kufikisha
huduma na mahitaji muhimu kwa Watanzania.
“Chama hichi
wakati wote kimesimamia utekekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi, kinafikisha huduma ambazo wewe mtanzania kila ukiamka ni lazima
uzitumie, chama hiki pia kimeendelea kusimamia amani
na utulivu nchini.”
0 Maoni