Mloganzila kufanya kambi ya kupunguza mafuta mwilini Feb 20-27, 2025

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji Rekebishi kutoka nchini India Dkt. Shraddha Deshpande inatarajia kufanya kambi maalum ya Upasuaji Rekebishi kuanzia Februari 20 hadi 27, 2025.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Eric Muhumba amesema lengo la kambi hiyo ni  kusaidia kupunguza mafuta kwa watu ambao wana mafuta mengi mwilini ili kuwapunguzia athari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la juu la damu pamoja na magonjwa ya moyo.

“Hii ni kambi yetu ya sita, tumeshawafanyia wagonjwa zaidi ya 50 na matokeo yamekuwa mazuri hivyo kutokana na uhitaji kuwa mkubwa tumeona ni vyema kufanya kambi nyingine ili kuwapunguzia watu usumbufu wa kwenda kupata huduma hii nje ya nchi,”ameeleza Dkt. Muhumba.

Chapisha Maoni

0 Maoni