SERIKALI ya
Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea
kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanapata
mitaji, leseni na matumizi ya teknolojia katika shughuli za uchimbaji wa madini
na kuwezesha kuchimba kisasa.
Akizungumza
katika mahojiano maalum mmiliki wa Mgodi wa Kwasakwasa uliopo kijiji cha
Msesule kata ya Mapogoro, wilayani Mbarali mkoani Mbeya, mwanadada Amagite
Mkumbwike amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mazingira wezeshi ikiwemo
bei nzuri sokoni ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika zaidi.
“Nikiwa
mchimbaji mdogo na mmiliki wa mgodi wa Kwasakwasa, nitaendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kuendelea kutoa
ajira kwa vijana na kurudisha faida kwa kile kinachopatikana katika vijiji
vinavyozunguka mgodi wetu,”amesema na kuongeza.
“Serikali
imerahisisha vitu vingi ikiwemo kuhakikisha bei ya dhahabu sokoni zinakuwa juu
ili wachimbaji wadogo tunufaike. Tumeendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa
kurudisha faida kwa jamii ikiwemo kununua vifaa vya shule kwa wanafunzi wa
kijiji hiki ambao wameendelea na masomo yao ya elimu ya juu, pamoja na kununua
mashine ya umwagiliaji hapa kijijini,”amesema Amagite.
Aidha, kwa
upande wa Msimamizi wa Mgodi huo Edward Daud ameiomba Serikali kuendelea kuweka
mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji ili vijana wengi wapate ajira kutokana na
uwekezaji unaofanywa.
“Na sisi
vijana tunapoaminiwa sehemu yoyote ile tukapewa kazi basi tuifanye kwa bidii
kwa asilimia 100, tuwe waaminifu kwa waliotupa dhamana,”amesema.




0 Maoni