Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini ili kuendelea kuwavutia wawekezaji.
Ameyasema
hayo leo, (Jumatano 12 Februari 2025) alipokutana na Ujumbe wa Wafanyabiashara
kutoka Falme ya Saidi Arabia, Katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu magogoni jijini
Dar es Salaam.
Mheshimiwa
Majaliwa amesema uhusiano baina ya Tanzania na Saudi Arabia umeendelea
kuimarika na kufungua fursa kwa wawekezaji kutoka Saudi Arabia kuwa na wigo wa
kuwekeza nchini Tanzania hususan katika sekta za nishati, Kilimo, Viwanda,
Mifugo Utalii na biashara.
Aidha,
amesema Tanzania imeendelea kunufaika na fursa ya kusafirisha bidhaa za mazao
na mifugo kwenda nchini Saudi Arabia jambo ambalo limeendelea kukuza uchumi wa
nchi.
Katika hatua
nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji hao kuwekeza katika
sekta ya nishati ili kuongeza nguvu katika kampeni ya nishati safi ya kupikia
iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
"Serikali
yetu imeweka mkazo katika kufikia malengo ya kuwawezesha wananchi kutumia
nishati safi ya kupikia na kuepukana na matumizi ya nishati zisozo rafiki kwa
mazingira, Nchi yetu bado ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya
nishati. Ninawakaribisha sana."

0 Maoni