Siku adhimu kwa
ajili ya kuwakutanisha wapendanao almaarufu Valentine's Day inaendelea vyema
ndani ya Hifadhi ya urithi wa utamaduni wa dunia ya Magofu ya Kale ya Kilwa
Kisiwani na Songo Mnara ambapo watalii kutoka sehemu mbalimbali wapo ndani ya
Hifadhi hiyo wakisheherekea Kwa kubarizi ndani ya boti la kisasa lijulikanalo
Kwa jina la TAWA SEA CRUISER.
Kadri muda
unavyosonga ndivyo Idadi ya watalii inavyozidi kuongezeka kwa Kasi na Mamlaka
ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kupitia Hifadhi hiyo inatarajia kupokea wageni
wengi siku ya leo kutokana na
mvuto wa Hifadhi hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa ikipokea Idadi kubwa ya
watalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani na watalii wa ndani.
TAWA
inaendelea kuwakaribisha watu wote kutembelea hifadhi hiyo kujionea vivutio vya
kihistoria na kiutamaduni ikiwemo kufurahia mandhari nzuri za fukwe pamoja
kuona viumbe vya majini kupitia TAWA SEA CRUISER.
0 Maoni