Viongozi wa Idara mbalimbali ndani ya Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wanafanya mafunzo maalum ya siku tatu kuanzia leo hadi tarehe 31, Januari 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara kuhusu Uhamasishaji wa Usimamizi wa Vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaji kazi wa TANAPA (Risk Management).
Akifungua mafunzo hayo Naibu Kamishna wa Uhifadhi na
Maendeleo ya Biashara, Massana Mwishawa aliwataka viongozi hao kutoka Makao
Makuu ya Shirika kutambua jukumu kubwa la kusimamia na kupunguza vihatarishi
ili kutekeleza majukumu ya Shirika kwa ufanisi mkubwa.
“ Lengo la mafunzo haya ni kuwapatia zana za vitendo,
maarifa, na mikakati ambayo itatumika kuboresha usimamizi wa vihatarishi katika
taasisi nzima. TANAPA tuna tekeleza muongozo wa usimamizi wa viatarishi
(Enterprise Risk Management Framework and Policy 2024/2025 - 2028/2029).”
“Mafuzo ya leo yameandaliwa ili kuongeza uelewa wetu kuhusu
umuhimu wa usimamizi wa vihatarishi, sio tu kama kazi, bali kama chombo cha
kimkakati kinacholingana na malengo yetu na kuboresha michakato yetu ya maamuzi.”
Aidha, Kamishna Mwishawa aliongeza kuwa vihatarishi ni jambo
lisiloweza kuepukika. Hivyo, ni muhimu kila mmoja wetu hasa wale walioko katika
nafasi za uongozi kuwa na uelewa thabiti wa jinsi ya kushughulikia changamoto
hizi kwa ufanisi na kusisitiza maandalizi ya bajeti za mwaka wa fedha 2025/2026
inapaswa kuzingatia vihatarishi, pamoja na hatua na mikakati ya kupunguza
vihatarishi yaani “Risk based budgeting”.
Mafunzo haya ya siku tatu ya usimamizi wa vihatarishi
yanaendeshwa na Dkt.Bernard Mnzava kutoka Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM).
Na. Edmund Salaho -Ziwa Manyara
0 Maoni