Leo tarehe 27 Januari 2025 Ikiwa ni kumbukizi ya siku
kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, TFS kupitia Shamba la Miti Saohill imeshiriki katika kampeni ya
"Mti wa Mama" kwa kupanda miti katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji
Mafinga iliyopo Wilayani Mufindi.
Katika kampeni hiyo jumla ya miti 500 ya aina mbalimbali
imepandwa katika Hospitali hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Mafinga
na wadau mbalimbali wa mazingira huku miche 400 kati ya hiyo ikitolewa na TFS.
Akizungumza katika kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Mhe.Dkt Linda Salekwa amesema kuwa kampeni hiyo hiyo imefanyika ikiwa ni
kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Rais na kuendelea kuunga mkono
juhudi za serikali ya awamu ya sita katika utunzaji wa mazingira.
Aidha ameipongeza TFS kwa kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi
kwa wananchi na kuhamasisha upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya
Mufindi kwani imekuwa ikileta tija kubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza
upatikanaji wa malighafi na uzalishaji wa mazao ya misitu.
Kampeni hiyo imeratibiwa na Kampuni ya Preshdas ambao ni wadau wa sekta ya kilimo cha miti na ufugaji nyuki na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Halmshauri ya Mji Mafinga akiwepo Mkurugenzi Bi Fidelisia Myovela, watumishi kutoka halmashauri na wadau mbalimbali ambapo kwa mwaka 2025 Halmashauri ya Mji Mafinga ina malengo ya kupanda miti takribani Milioni moja.
0 Maoni