Dkt. Biteko atoa pole kwa Wanabukombe kufuatia ajali ya radi

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ametoa salamu za pole kutokana na ajali ya radi iliyosababisha vifo vya wanafunzi saba wa Shule ya Sekondari ya Businda, iliyopo wilaya ya Bukombe Mkoani Geita na kujeruhi wengine 82.

Katika salamu zake hizo za pole Dkt. Biteko amesema, “Nimepokea taarifa ya vifo vya watoto wetu wa Businda sekondari kwa masikitiko makubwa.”

Dkt. Biteko ametoa pole kwa wazazi, walezi, walimu, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Businda na ndugu wote waliguswa na msiba huu mkubwa.

Vifo vya vijana wetu vimetushtua sana wana Bukombe wote, amesema Dkt. Biteko ambaye ni mbunge wa Bukombe.

“Tunawaombea faraja familia zote zilizofikwa na msiba huu aidha, tunawaombea uponyaji wa haraka majeruhi wote kwenye kadhia hii,” alisema Dkt. Biteko

Nimemuomba Mhe. Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Ofisi ya Mbunge kufuatilia kwa karibu matibabu ya majeruhi wote na taratibu za mazishi ya watoto wetu wapendwa waliotangulia mbele ya haki, imemalizia taarifa hiyo ya Dkt. Biteko.



Chapisha Maoni

0 Maoni