Serikali imekemea watanzania wanao kwenda kufanya kazi nje
ya nchi bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa
inasababisha kutojulikana walipo na shughuli wanazozifanya.
Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa
uzinduzi wa utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu Ajira za
Watanzania nchini Saudi Arabia.
Aidha, amesema uhusiano mazuri uliopo baina ya Tanzania na
nchi ya Saudi Arabia hawataruhusu wafanyakazi kufanya kazi au kusafiri bila
kufuata utaratibu, hivyo kila mtanzania anayehitaji kufanya kazi nje ya nchi
apitie kwa mawakala wanatambulika baina ya nchi hizo mbili.
Mhe. Ridhiwani amesema miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa watanzania kusafiri kwenda nchini Saudi Arabia, upimaji wa Afya zao, kupata kazi zenye staha na mshahara mzuri ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi.
0 Maoni