Rais Samia awaonya wanaoanza kampeni mapema

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewaonya wanachama wa CCM wenye nia ya kugombea nafasi za udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka 2025 ambao wameanza kupita pita majimboni na katika kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati.

Dk. Samia ametoa onyo hilo leo Januari 18,2025 jijini Dodoma ambako kunafanyika Mkutano Mkuu maalum kwa ajili ya kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2024 ubunge na udiwani ambao wameanza kampeni za mapema kabla ya wakati.

Akieleza kuhusu walioanza kampeni kabla ya wakati, Dk. Samia amesema kwamba chama kimepata ushahidi ambao unaonesha wapo baadhi ya watu wakiwakusanya wananchi kwa madai ya kuwawezesha kupitia shughuli za kijamii lakini lengo ni kutaka kujitambulisha kwa wapiga kura.

“Wanachama wenye tabia ya kuendeleza makundi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu badala ya kuwaunga mkono wagombea waliopitishwa na chama….kwa wale ambao wamejipanga kugombea wasubirie wakati ufike.”

“Tumeshapokea malalamiko na ushahidi wa picha za watu wanaofanya misafara kwenda majimboni, wanaitisha mikutano ya jimbo kwa kigezo cha ufungaji ila malengo yao ni kujitambulisha kwa wanachana,” alisema Rasi Dk. Samia na kuongeza kwa kutoa onyo, “Nawaonya wote wenye tabia hii kuacha mara moja.”

Chapisha Maoni

0 Maoni