Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali
katika Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira ameteuliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa bara.
Wasira ambaye jina lake limewasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu
Maalum wa CCM unaoendelea jijini Dodoma leo Januari 18, 2025, limepata baraka
za Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kuchukua nafasi
iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana aliyetangaza kupumzika miezi mitano
iliyopita.
Kwa sasa jina la Wasira litapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.
0 Maoni