Wasira kuanza na 4R za Rais Samia baada ya kuchaguliwa

Kada mkongwe wa CCM Stephen Wasira amesema moja ya kitu anachotarajia kuanza nacho kama Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) baada ya kuchaguliwa ni kuendeleza maridhiano kwa sababu maridhiano ni jamii.

Wasira amesema hayo leo Jumamosi Januari 18, 2025 wakati akizungumza mkutano mkuu wa maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma leo Jumamosi Januari 18, 2025.

Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, unaoendelea jijini Dodoma ulimchagua kwa kishindo  Stephen Masato Wasira, kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara kwa kupata zaidi ya kura 99% za wajumbe.

Katika mkutano huo, kura 1921 zilipigwa, ambapo kura halali zilikuwa 1917. Kura za hapana zilikuwa 7, na kura za ndiyo zilikuwa 1910, sawa na  asilimia  99.42% huku Kura 4 zikiharibika.

Chapisha Maoni

0 Maoni