Mtandao wa TikTok haupatikani nchini Marekani, saa chache
kabla ya sheria mpya ya kupiga marufuku jukwaa hilo la mtandao wa kijamii kuanza
kutumika.
Ujumbe unaoonekana kwenye programu kwa watumiaji wa
Marekani unasema sheria ya kupiga marufuku TikTok imepitishwa, ukimaanisha
"huwezi kutumia TikTok kwa sasa."
Tuna bahati kwamba Rais Trump amedokeza kuwa
atashirikiana nasi kutafuta suluhisho la kurejesha TikTok mara tu atakapoingia
madarakani, imesema taarifa ya TikTok.
Watumiaji waliripoti kuwa programu hiyo pia ilikuwa
imeondolewa kwenye Apple na Google ya Marekani huku TikTok.com haikuwa
inaonyesha video.
TikTok imesema kwamba sheria hiyo mpya inakiuka uhuru wa
kujieleza kwa watumiaji milioni 170 wa mtandao huo nchini Marekani.
0 Maoni