Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemshukuru Mwenyezi Mungu katika siku yake ya kuzaliwa hii leo. Rais Samia ameandika maneneno yafuatayo kupitia akuanti yake ya mtandao wa X:-
Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa neema na
baraka zake leo ninapotimiza umri wa miaka 65. Sifa njema zote ni zake Yeye,
Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Nawashukuru nyote kwa salamu nyingi za kheri na upendo kwa
siku hii, na kwa dua njema katika kazi ya kulitumikia Taifa letu.
Ahsanteni sana.
0 Maoni