Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy
Chakwera, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa
Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unafanyika
tarehe 27 na 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius
Nyerere.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Mheshimiwa Dkt. Chakwera alilakiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha
na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Saada Mkuya, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi na maafisa waandamizi wa
serikali.
Mkutano huo unawaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, wataalam wa nishati, viongozi wa sekta binafsi, na washirika wa maendeleo kwa ajili ya kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto za nishati na kuchangamkia fursa za bara la Afrika. Moja ya matokeo muhimu ya mkutano huo ni kupitishwa kwa Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya pamoja ya viongozi wa Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya bara hili.
0 Maoni