Wageni wengi wametembelea eneo la Mnara wa Saa "Clock
Tower" kwa ajili ya kujionea taswira mbalimbali za wanyamapori pamoja na
kupata elimu kuhusu umuhimu wa kijiografia wa eneo hilo.
Uwepo wa Taswira za Wanyamapori ambazo zimewekwa na TAWA
katika eneo hilo limenogesha zaidi kwa kuwavutia wageni wengi wazawa na wasio
wazawa kutembelea eneo hilo na kupiga picha.
Uzuri wa eneo hilo kwa sasa, umevutia watu wengi kuchukua
matukio mbalimbali kama vile kurekodi video, kupiga picha za sherehe n.k
Watu wengi wamepongeza uongozi wa Mkoa wa Arusha na
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA kwa kuhakikisha watanzania
wanafurahia rasilimali za wanyamapori zilizopo.
0 Maoni