Kamati ya Siasa CCM mkoa Dodoma yatembelea Hifadhi ya Mikumi

 

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Ndugu Charles Saimon Mamba, wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa lengo la kujifunza na kujionea vivutio vya wanyamapori na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa.

Katika ziara hiyo walioifanya jana, kamati ilipata fursa ya kushuhudia wanyamapori mbalimbali kama vile tembo, simba, twiga, na pundamilia.

Aidha walitembelea miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma za utalii, ambayo imetekelezwa kwa fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukuza utalii wa ndani na kimataifa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo alisifu juhudi za serikali na TANAPA katika kuboresha miundombinu na kuhifadhi maliasili, akiwahimiza Watanzania kuendelea kuthamini na kutembelea hifadhi za taifa.



Chapisha Maoni

0 Maoni