Mwanaume mmoja amekamatwa Jijini New York nchini Marekani
kwa kuhusika na kifo cha mwanamke aliyechomwa moto kwenye treni ya aridhini.
Kamishna wa Polisi Jessica Tisch ameelezea tukio hilo la
Jumapili kama moja ya matukio ya kihalifu ambayo mtu huwezi kuamini anaweza
kumtendea binadamu mwenzake.
Kamishna Tisch ameeleza kuwa mwanamke huyo akiwa kwenye
treni iliyosimama huko Brooklyn alifuatwa na mwanaume huyo aliyetumia kibiriti
kuwasha moto nguo zake.
Amesema mwanamke huyo alikufa papo hapo kwenye treni, na
kuongeza kuwa mhusika amekamatwa. Hakukua na maongezi yoyote baina yao kabla ya
kuchomwa moto.
0 Maoni