Wadau kutoka Estonia wavutiwa na banda la TAWIRI

  

              

Wanasayansi kutoka nchi ya Estonia, ni miongoni mwa wadau ambao wameendelea kutembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) katika Maonesho ya Kongamano la Kimataifa la TAFORI linaloendea kwa siku ya pili katika ukumbi wa AICC- Arusha.

TAWIRI tunakukaribisha ujifunze kuhusu tafiti za wanyamapori, mbinu za kudhibiti migongano kati ya binadamu na Wanyamapori, ufugaji bora wa nyuki na uongezaji thamani mazao ya nyuki, uvumbuzi na matumizi ya teknolojia rafiki katika uhifadhi, Sensa za Wanyamapori, Matibabu ya Wanyamapori, pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya Uhifadhi na Utalii.



Chapisha Maoni

0 Maoni