Fury asema majaji wamempa zawadi ya Krismasi mpinzani wake

 

Bondia Tyson Fury amegoma kukubali kupoteza pambano la marudio la mikanda ya uzito wa juu dhidi ya Oleksandr Usyk, na kudai majaji wamempa “Zawadi ya Krismasi” mpinzani wake.

Majaji wote watatu walimpa alama 116-112 bondia Usky, na kumfanya bondio huyo wa Ukraine kupata ushindi wa pili mfululizo dhidi ya mpinzani wake Muingereza Tyson Fury.

Hata hivyo Fury pamoja na promota wake Frank Warren wamekuwa wagumu kukubali ushindi huo wakiamini walistahili ushindi katika pambano hilo lililofanyika Riyadh, Saudi Arabia.

“Najua nilipaswa kumpiga kwa knock out, hizi ni ngumi na hiki ndicho kilichotokea. Sina shaka kwenye akili yangu nimeshinda hili pambano,” amesema Fury.

Chapisha Maoni

0 Maoni