Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia asubuhi ya leo tarehe 20/11/2024 watu 20 wamefariki kutokana na maafa ya ghorofa lililoporomoka Kariakoo, Dar es Salaam.
Rais Samia
ametoa kauli hiyo leo alipofika katika eneo la tukio hilo Kariakoo, ikiwa ni muda
mfupi tu baada ya kurejea kutoka nchini Brazil, ambapo amekagua shughuli za
uokoaji na kisha kuongea na wananchi.
“Jitihada zetu kubwa katika tukio hili imekuwa
kuwaokoa wenzetu walionasa katika jengo hili wakiwa hai lakini kama tunavyoambiwa
jitihada haziondoshi kudra ya Mungu, pamoja na jitihada tulizofanya kuna
wenzetu tumewapoteza,” alisema Rais Samia kwa huzuni.
“Hili sio pigo kwa familia zilizopoteza eatu
wao pekee yao ni pigo letu kama Watanzania na tunaguswa pia, ni kumbukumbu ya
kutisha kwa wenzetu waliookoka hapa, kwa jinsi jengo lilivyo mtu akitoka hai
bila shaka hawapo sawa kisaikolojia, niombe wasifadhaike, wajipe moyo na tuendelee
na shughuli zetu za kawaida bado Mungu ana kazi nao.”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.




0 Maoni