Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahamasisha
wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la uchaguzi wa serikali za
mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba 2024.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati
akizungumza na abiria waliosafiri pamoja naye kwa kutumia usafiri wa ndege ya
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani
Kigoma leo tarehe 26 Novemba 2024.
Amewasihi
wananchi waliojiandikisha kuchagua viongozi bora katika uchaguzi huo.
0 Maoni