Mbunge wa
Kigamboni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Faustine Ndugulile
amefariki dunia leo Novemba 27, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya
kifo chake iliyotolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson, imesema
taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadae.
Dk.
Ndugulile alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika
(WHO) ambaye alitarajiwa kuanza rasmi majukumu yake hayo mapya Februari mwakani.
0 Maoni