Watanzania
katika maeneo mbalimbali ya nchi wamejitokeza kupiga kura kwa ajili ya
kuwachagua viongozi wao ngazi ya Serikali za Mitaa.
Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametimiza haki yake ya
Kikatiba katika Kata ya Bulangwa, Wilayani Bukombe, Geita kisha akawashukuru
wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Dkt. Biteko
amesema hayo leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kupiga kura katika kituo cha
kupiga kura cha Shule ya Msingi Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita.
“Zoezi la
kupiga kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi nawapongeza
kwa hilo. Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti kwa sababu ya hamasa kubwa ya
kushiriki,” amesema Dkt. Biteko.
Amesisitiza
“Ninaomba watu wote waliojiandikisha watumie haki yao ya kikatiba kwa
kujitokeza kwa wingi na kwenda kupiga kura.”
Kampeni za
uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizinduliwa Novemba 20, 2024 na kuhitimishwa
Novemba 26, 2024 baada ya wagonbea kujinadi na kuomba kura kwa wananchi.
0 Maoni