Rais Mstaafu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo ameshiriki
zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji
katika kijiji cha Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Pwani ikiwa
ni haki ya msingi ya kumpata kiongozi aneedhani kuwa ataleta maendeleo katika
kijiji chake.
Mh. Kikwete aliwasili
majira ya saa nne asubuhi katika kituo cha Kota kilichopo kijiji cha msoga na
kupiga kura ikiwa ni sehemu ya kutekeleza demokrasia inayolenga kumpata
mwenyekiti na wajumbe huku akieleza kufurahishwa na idadi ya wananchi
waliojitokeza kupiga kura kwani hii inaonesha namna wananchi walivyohamasika
kushiriki katika uchaguzi.
Mbunge wa
jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete kufurahishwa na utaratibu mzuri uliowekwa na
serikali ya kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani na utulivu.
Mmoja wa
wagombea katika uchaguzi huo Hasasan Shaban akaeleza kuwa kutokana na kijiji
hicho kutokua na wagombea kwa upande upindi matumaini yake kuwa ataibuka na
ushindi kwa kupata kura nyingi za ndio ili awatumie
wananchi wa eneo hilo.
0 Maoni