Jeshi la
Polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Martin Hyera kwa kosa la kumuua mke wake Luciana
Kapinga kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani chanzo kikiwa kunyimwa unyumba.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Ruvuma SACP Marco Chilya amesema kuwa, tukio hilo limetokea tarehe
Novemba 14, 2024 majira ya saa 12 asubuhi katika kitongoji cha mbilo kijiji cha
kizuka kilichopo kata ya kizuka tarafa ya Mhukuru Wilayani Songea.
Ameeleza
kuwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la Luciana Dastani kapinga (22) mkulima
mkazi wa kitongoji cha mbilo aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito chenye ncha
kali maeneo ya kichwani upande wa juu wa jicho la kushoto hadi kichwa kubonyea
na mume wake aitwaye Martin Hyera baada ya kumnyima unyumba.
"Wawili
hao walionekana alfajiri wakikimbizana huku mtuhumiwa Martin Hyera akiwa
ameshika mpini wa shoka kisha kutekeleza mauaji hayo na baada ya mauaji hayo mtuhumiwa
alimpigia simu shangazi yake aitwaye Paulina Nchimbi na kumjulisha kuwa amemuua
mke wake kwa sababu amekuwa akimnyima unyumba kwa muda mrefu kisha mtuhumiwa akatoroka,"
amesema Kamanda Chilya.
0 Maoni