COSTECH yahitaji kazi za ubunifu katika teknolojia

 

Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), imetoa wito kwa wabunifu nchini kupeleka kazi zao za kibunifu kwenye teknolojia ili waweze kunufaika.

Akizungumza kwenye kikao na Wahariri leo, Meneja wa NFAST Dk. Beatrice Lymo, amesema, moja ya kazi ya tume hiyo ni kushindanisha kazi za wabunifu katika teknolojia lakini pia kutoa mikopo.

“Kati ya kazi za tume ni kushindanisha wabunifu katika teknolojia, sayansi na tafiti. Natoa wito kwa wabunifu kuleta kazi na maandiko yao COSTECH ili waweze kunufaika na mikopo pamoja na mitaji,” amesema.

Dk. Lyimo amesema, tume hiyo itaingia makubaliano na benki kwa ajili ya kuanzisha Mfuko wa Mikopo ili kusaidia upatikanaji wa mikopo kwa wabunifu na wavumbuzi.



Chapisha Maoni

0 Maoni