Wanahabari kupewa kipaumbele upimaji na matibabu ya moyo bila malipo Kliniki ya JKCI

 

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Peter Kisenge watatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Taarifa iliyotolewa leo na JKCI imesema huduma hiyo itatolewa bila malipo kwa watoto na watu wazima wakiwemo Waandishi wa Habari lengo likiwa ni kusogeza huduma za kibingwa za matibabu ya moyo karibu zaidi na wananchi.

Matibabu haya yatatolewa tarehe 29-30/10/2024 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Kliniki ya JKCI Kawe iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health Plaza barabara ya Tuari, imeeleza taarifa hiyo.

JKCI imewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kujua kama wana matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0783922571 na 0680280007.

   "Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu".


Chapisha Maoni

0 Maoni