Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida leo Oktoba 28,2024 kwa ajili ya kupatia ufumbuzi changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo katika Wilaya hiyo.
Mhe. Chana amepokelewa na Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi, Mhe.Thomas Apson
ambapo pamoja na mambo mengine amepokea
taarifa kuhusu hali ya udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu Mkoani
Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima
Dendego akizungumza katika kikao cha awali ametoa maelezo kuhusu tukio la tembo
lililotokea katika eneo la Kambi ya Mkaa Wilayani Ikungi Oktoba 26,2024 ambalo
lilisababisha taharuki kwa wananchi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Alex
Lobora, Kamishna Uhifadhi Msaidizi Mwandamizi na Mkuu wa Kanda ya Kati, Herman
Nyanda pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii, TAWA na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.
Na. Happiness Shayo- Singida
0 Maoni