Tanzania, Kenya kushirikiana katika sekta ya utalii

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Isaac Njenga pembezoni mwa Onesho la Kimataifa la Swahili International Tourisim Expo-S!TE (S!TE 2024) jijini Dar es Salaam.

Lengo la kikao hicho kilichofanyika jana ni kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano katika Sekta ya Maliasili na Utalii baina ya nchi za Kenya na Tanzania.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dkt. Ramadhan Dau, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkuba Mabula, Mkurugenzi Mkuu Bodi za Utalii Tanzania(TTB), Ephraim Mafuru na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt. Thereza Mugobi.

Chapisha Maoni

0 Maoni