Tajiri wa India mmiliki wa kampuni ya Tata afariki dunia

 

Tajiri mkubwa nchini India mmiliki wa kampuni ya Tata inayojulikana kwa magari yake ya Tata, Ratan Tata amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, taarifa ya makampuni ya Tata imetangaza.

Ratan Tata ni mmoja wa mfanyabiashara wa India anayetambulika kimataifa na makampuni ya Tata ni miongoni mwa makampuni makubwa mno nchini India.

Katika uongozi wake Tata alinunua bidhaa za hali ya juu za Uingereza kama Jaguar, Land Rover pamoja na kampuni kubwa ya pili ya chai duniani ya Tetley.

Katika salamu zake za rambirambi Waziri Mkuu wa Uingereza Narendra Modi, amemuelezea Tata kuwa ni mfanyabiashara mwenye maono, mwenye roho ya upendo na ubinadamu wa hali ya juu.

Makampuni ya Tata yaliyoanzishwa mwaka 1868, ni moja ya makampuni makubwa yanayouza bidhaa na kutoa huduma zake kwa mataifa 150 duniani na kufanya shughuli zake kwenye mataifa 100.

Chapisha Maoni

0 Maoni