Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema amani na mshikamano wa
Watanzania unapaswa kuwa mojawapo ya vipaumbele kwa kila Mtanzania.
Balozi Nchimbi amesema kuwa wasisi wa
Taifa la Tanzania na wazee walifanya kazi kubwa katika kuweka misingi ya
kulinda na kutunza amani ya nchi, wakitumia hekima na uzoefu ili kuhakikisha
kuwa jamii ya Watanzania inakuwa na mshikamano siku zote.
“Ni jukumu letu sasa kuendeleza amani
hiyo na thamani yake kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni muhimu kutunza umoja wetu
na kushirikiana kwa pamoja. Tunapaswa kudumisha na kujenga mazingira ya amani
na ushirikiano. Umoja ni nguvu.”
“Hatupaswi kukubali kuharibiwa umoja
wetu. Tunapaswa kufanya kazi pamoja ili kulinda amani na kutatua tofauti zetu
kwa njia ya mazungumzo na kuelewana. Umoja wetu ni msingi wa nguvu na amani,”
amesema Balozi Dkt. Nchimbi.
Balozi Nchimbi ameyasema hayo wakati
akizungumza na wananchi wa eneo la Tinde mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku ya
kwanza ya ziara yake ndani ya mkoa huo, akiongozana na Katibu wa NEC-Itikadi
Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia
0 Maoni