Kimbunga Milton chasababisha maafa Florida

 

Kimbunga Milton kimeikumba jimbo la Florida nchini Marekani kikisababisha mafuriko na kutishia kuongezeka kwa gharika.

Nyumba zaidi ya milioni moja na maeneo ya biashara yamekosa umeme na kuna taarifa za kutokea vifo katika Pwani ya Atlantic.

Huko St Perersburg, pwani ya magharibi ya jimbo hilo, paa la uwanja wa ligi ya mpira wa baseball limepasuka kwa upepo mkali.

Kimbunga Milton kilichokuwa na kipimo cha daraja la tano, kimeshushwa daraja hadi kufika la kwanza, hata hivyo bado kina madhara.



Chapisha Maoni

0 Maoni