Serikali kupitia Maonesho ya Swahili International Tourism Expo- S!TE imezidi kufungua milango ya fursa katika sekta ya Utalii zinazopatikana nchini kwa wadau mbalimbali wa Utalii wa ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili
na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) leo Oktoba 13, 2024 Jijini Dar es
Salaam, alipofunga rasmi Onesho la
Kimataifa la Utalii la Swahili International Tourism Expo ambalo limedumu kwa
siku ya tatu.
Waziri Chana amesema kuwa Onesho hilo
ni matokeo chanya ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika jitihada zake za kuibua fursa kwenye sekta ya
Utalii nchini ili watanzania waweze kuzichangamkia kwa lengo la Kuboresha
maisha yao na kuinua uchumi wa nchini.
Mhe. Chana amewapongeza wadau wote wa
Utalii walioshiriki katika maonesho hayo na kuahidi kuwa Wizara ya Maliasili na
Utalii kupitia Bodi ya Utalii nchini itaendelea kushirikiana vyema na wadau
wote wa ndani na nje katika kuhakikisha sekta ya Utalii inakuwa zaidi kwa
maslahi mapana ya Taifa.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania, Balozi Dkt. Ramadhan Dau, ameushukuru
uongozi wa Wizara kwa kazi kubwa inayofanya ya kukuza na kuendeleza Utalii
nchini na kwamba TTB itaendelea kutekeleza majukumu yake ya kutangaza Utalii
ndani na nje ya nchi.
Akizungumza kwa niaba ya wanunuzi wa
bidhaa za Utalii waliohudhuria Onesho hilo, Reno Mauricio kutoka nchini Ureno
ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa mazingira mazuri ya uwekezaji iliyoweka kwa
wadau wa Utalii kutoka nje ya Tanzania hali inayopelekea wengi kuchangamkia
fursa zilizopo nchini.
Maonesho hayo Makubwa ya Utalii,
yamewakutanisha wanunuzi wa bidhaa ya Utalii zaidi 120 na nchi washiriki
takribani 50 yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe Dkt. Hussen Ali Mwinyi.
Na. Happiness Shayo- Dar es Salaam
0 Maoni