Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan kwa usimamizi madhubuti wa sekta unaopelekea ukuaji wa haraka wa mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa.
Hayo yameelezwa leo Oktoba 13, 2024 na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati
akifunga maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.
Aidha Mhe. Rais Samia ameeleza katika
mikakati ya kuimarisha uchumi wa nchi na upatikanaji wa fedha za kigeni
Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetenga kiasi cha shilingi
Trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji.
Rais, Dkt. Samia amesema kwamba sekta
ya madini imekuwa na mchango mkubwa katika kuliingizia taifa fedha za kigeni
ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilichangia asilimia 56 ya fedha za kigeni.
Sambamba na hapo Rais Dkt. Samia
amesema kiasi cha shilingi 250 zimetengwa kama dhamana ya mikopo zitakazo
wawezesha wanunuzi wa dhahabu kupata mtaji.
Rais Dkt. Samia amesema kuwa, kwa mwaka wa 2023 mauzo ya madini yenye
thamani ya zaidi ya shilingi trilioni mbili yaliuzwa katika masoko 44 na vituo
mbalimbali vya uuzaji madini vilivyopo
sehemu mbalimbali nchini.
Akielezea kuhusu mwenendo wa biashara ya
madini nchini kuanzia mwaka 2019 mpaka septemba 2024 , Dkt.Samia amesema kwa
kipindi husika kiasi cha tani 20.8 za dhahabu zenye gharama ya shilingi
trilioni 5.2 zimenunuliwa kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara ya madini
nchini.
Dkt. Samia ameeleza serikali inatambua
mchango wa asilimia 40 kutoka kwa wachimbaji wadogo nchini, ambapo ametoa
leseni 21 kwa vikuandi vya Vijana na wanawake
vikiwemo vikundi vya GEWOMA , Ushirika Madirisha na TEWOMA
vinavyojihusisha na uchimbaji mdogo.
Naye, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameipongeza wizara ya madini kwa juhudi mbalimbali
inazofanya za mageuzi katika mnyororo wa thamani katika sekta ya madini hususan
katika masuala uongezaji thamani madini na mpango ya kufanya utafiti wa kina kwa
asilimia 50 ifikapo mwaka wa 2030.
Akielezea kuhusu mikakati iliyopo ndani
ya sekta ya madini, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema katika
kuimarisha uchimbaji wenye tija na uhakika Serikali itajenga Maabara kubwa
mkoani Dodoma na Geita ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupeleka sampuli zao
kwa ajili ya uchunguzi wa sampuli za
madini na miamba.
Waziri Mavunde amesema kuwa wizara
inaendelea kuweka mipango mizuri katika ukusanyaji wa maduhuli ambapo kwa
kipindi cha siku 90 cha mwaka wa 2024/2025 wizara kupitia Tume ya Madini imekusanya
kiasi cha shilingi Bilioni 287 ambayo ni zaidi ya asilimia 106.
Akielezea kuhusu utekelezaji wa Sheria
na Kanuni ndani ya Wizara, Waziri Mavunde amesema kuwa wizara imekuwa ikizingatia taratibu zote
za utekelezaji wa Mpango wa
Ushirikishwaji wa Jamii inayozunguka mgodi na Mpango wa Urudishaji kwa Jamii
ambapo kwasasa ipo na mpango mpya wa
Mining for Brighter Tommorrow (MBT) utakao washirikisha vijana na wakina mama.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la
Geita Mjini Mhe. Constantine Kanyasu amemshukuru Rais , Dkt.Samia kwa kupeleka
fedha za miradi ya maendeleo mkoani
Geita katika sekta ya Afya,Maji, Barabara na
Elimu.
Pamoja na mambo mengine, Rais wa
Shirikisho la Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMATA) John Bina amemuomba
Rais , Dkt. Samia kuifanya dira ya Vision2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri
kuwa kitaifa badala ya kisekta.
Kwa mara ya kwanza maonesho ya Saba ya
Teknolojia ya madini yamefungwa leo rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
0 Maoni