Mwanamke ajiteka ili amrudishe mumewe nyumbani

 

Mwanamke mmoja wa Mkazi wa Matalawe Mjini Njombe, Joyce Ojala (32), anashikiliwa na polisi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiojulikana ili kumlazimisha mumewe Mfaume Hussein Mzee (37), aliyekuwa Mkoani Ruvuma kwa zaidi ya miezi sita akifanya kazi za madini kurejea nyumbani.

Akisimulia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amesema Joyce alitoa taarifa kwa mumewe akidai ametekwa na kwamba mume wake anatakiwa kurudi haraka ili kushughulikia suala hilo.

Amesema baada ya Mfaume, kupokea taarifa hiyo na kuamua kurejea mara moja nyumbani baada ya kuambiwa kuwa mkewe yuko hatarini lakini alipofuatilia polisi ilibainika kuwa hakuna tukio la utekaji na kwamba mwanamke huyo alijiteka mwenyewe kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda Banga ameeleza kuwa mume huyo alikuwa akiwasiliana na mke wake mara kwa mara na kumjulisha kuwa anafanya shughuli za madini na hana uwezo wa kurudi mara moja hata hivyo mwanamke huyo aliingia wivu na kuamua kutengeneza kisa hicho cha utekaji ili kumfanya mume wake kurudi.

Chapisha Maoni

0 Maoni