Mbwa ang’ata mkono wa mmiliki wake na kuukata

 

Mwanamke mmoja nchini Australia anapigania uhai wake hospitali baada ya kung’atwa mkono na mbwa wake na kuukata kaskazini mwa Queensland.

Vikosi vya uokoaji vililazimika kuitwa kuokoa maisha ya mwanamke huyo katika mji wa pwani wa Twonville, na kumkuta akiwa katika hali mbaya.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34, mkono wake wa kulia ulikuwa na majeraha makubwa na kukatika kwenye sehemu ya kiwiko.

Polisi walilazimika kumpiga risasi na kumuua mbwa huyo aina ya pit bull ambaye alikuwa amefungiwa ndani ya nyumba huku akiwa na hasira kali.

Polisi wamesema walipowasili walimkuta mwanamke huyo akitokwa damu nje ya nyumba na mbwa wake akiwa ndani huku akihaha kutoka nje kwa hasira.

Chapisha Maoni

0 Maoni