Viongozi na wananchi mbali mbali
wameendelea kujitokeza upata elimu kuhusu madini yaliyopo katika miamba na
namna ya kupima sampuli za madini ya metali kwenye mashine ya XRF katika Banda
la Tume ya Madini katika Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye
Sekta ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita.
Mashine hiyo ni maalum kwa kupima
madini ya metali kwa njia ya mionzi /X-RAY na kisha kukupa majibu kwa
kukuonyesha kiwango cha madini yote yaliyomo ndani ya metali hiyo kwa asilimia.
Akitoa elimu hiyo kwa viongozi na
wananchi Afisa Maabara kutoka Tume ya Madini, Mhandisi Edith Lewis amesema kuwa
madini yapo ya aina nyingi duniani
lakini huwa hayakai yenyewe, lazima
yanakuwa yamechanganyikana na aina mbalimbali nyingine za madini katika miamba.
Amesema, watu wanaonunua dhahabu ambao
wanaogopa kutapeliwa kwa kuuziwa dhahabu feki wafike kwenye banda la Tume ya
Madini kupata elimu ya namna ya kutambua miamba na madini mbalimbali pia
wanaweza kupima hereni, mikufu ya dhahabu na shaba katika banda na kushauri wananchi kuitumia fursa hii kufika
katika maabara ya Tume madini iliyopo Msasani- Tirdo Complex jijini Dar es
Salaam ili kupima sampuli zao.
“Hii mashine ina kioo maalum
itakuonyesha kwenye kioo madini yaliyomo ndani mfano ukipima dhahabu baada ya
mionzi kuscan itakuonyesha dhahabu ipo asilimia 11 na Shaba ipo asilimia 89
sasa wewe ukiona hivi unajua moja kwa
moja ulichouziwa ni feki ama si feki.”
Amesema pia kuna mashine ya kupima
sampuli za miamba kwa njia ya mionzi ambayo inatoa majibu ya ‘elements’ zote
zilizomo kwenye huo mwamba na majina yake na wingi wake kwa kukuwekea asilimia
yaani kama ni shaba utaona itaandika
"Cu....%, kama ni madini ya chuma itaandika "Fe"....% kama ni
dhahabu ipo itaandika "Au"....%.
Aidha, Mhandisi Edith ametoa wito kwa
wananchi wanaofika kwenye maonesho ya Madini Geita kutembelea banda la Tume ya
Madini ili pia kujionea vito mbali mbali na kujifunza fursa zilizopo katika
sekta ya madini.
Kauli mbiu ya mwaka 2024 katika
Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ni ‘Matumizi
ya Teknolojia Sahihi na Nishati Safi katika Sekta ya Madini kwa Maendeleo
Endelevu’.
Baadhi ya viongozi waliotembelea Banda
la Tume ya Madini na kupata elimu ya upimaji sampuli ni Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, Mbunge wa Geita Mjini Constantine Kanyasu ambae
pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Viongozi wengine waliotembelea banda
la Tume ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela,
Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga, Mkurugenzi wa Blue Coast Ignas
Inyasi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt.
Venance Mwasse, Katibu Tawala wa Wilaya
ya Mbogwe, Dkt. Jacob Julius na
Mwenyekiti wa UVCCM Geita Manjale Magambo.
0 Maoni