Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili na kupokelewa rasmi Mkoa wa
Shinyanga, leo tarehe 9 Oktoba 2024, tayari kuanza ziara ya siku tatu katika maeneo
mbalimbali ya wilaya za mkoa huo.
Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Katibu
wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla, ameingia
Shinyanga akitokea Mkoa wa Simiyu, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kukagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kusikiliza kero na
changamoto za wananchi kisha kuzitafutia majawabu na kuhamasisha uimara wa CCM
kuanzia ngazi ya mashina.
0 Maoni