Balozi Mshana akutana na Waziri wa Michezo wa DRC

 

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mheshimiwa Said mshana amekutana na kuzungumza na Waziri wa Michezo na Burudani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Didier Budimbu Ntubuanga.

Kikao hicho kimefanyika Ofisini kwa Mhe. Waziri Ntubuanga jijini Kinshasa

Mhe. Balozi alikwenda kuonana na Mhe. Waziri kwa ajili ya kumshukuru kwa mapokezi mazuri ambayo Serikali ya DRC imeipatia timu ya Taifa ya Tanzania iliyoko nchini DRC kwa ajili ya mchezo wake na timu ya Taifa ya DRC unaotarajiwa kufanyika tarehe 10 Oktoba 2024 jijini Kinshansa nchini DRC.

Taifa Stars inakutana na Timu ya Taifa ya DRC maarufu kwa jina la Chui, kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kufanyika nchini Morroco mwaka 2025.

Chapisha Maoni

0 Maoni