Mamilioni ya wakazi Florida kuondoka kupisha kimbunga

 

Mamilioni ya watu waliopo Florida nchini Marekani wanaharakisha kuondoka kwenye nyumba zao, wakati kimbunga Milton kikielekea kulikumba jimbo hilo la pwani ya mashariki.

Kimbunga Milton chenye ukubwa wa daraja la tano, kinatarajiwa kulikumba eneo la Tampa usiku, kikiambatana na upepo mkali wenye kasi ya kilomita 270 kwa saa.

Rais wa Marekani Joe Biden ameonya na kusema kuwa kuondoka ni suala la “uhai na kifo”, wakati jimbo hilo likifanya jitihada za kuhamisha idadi kubwa ya watu kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.




Chapisha Maoni

0 Maoni