RC Babu atoa maagizo kwa Maafisa Tarafa

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Mhe. Nurdin Babu amewasisitiza Maafisa Tarafa Mkoani Kilimanjaro kuhakikisha wanashughulikia kero na malalamiko ya Wananchi katika maeneo yao.

Mhe. Babu ameyasema hayo jana wakati akihitimisha mafunzo  ya siku mbili  kwa Maafisa Tarafa yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 

Aidha,  amewataka Maafisa hao kuzingatia misingi yao kwa kufuata Sheria, Kanuni na Maadili ili kuhakikisha kero za wanachi zinapata ufumbuzi kwa wakati.

Chapisha Maoni

0 Maoni