Mashirika ya umma kuingia kwenye masoko ya nje

 

Mashirika ya Umma ya Tanzania na yale ya binafsi yenye uwekezaji wa Serikali, sasa yataanza kupanua uwekezaji wao kwenye masoko ya nje ili kutoa huduma na kuongeza faida kwa taifa.

Hatua za kimkakati za Mwana Mageuzi waTanzania na Mwasisi wa Falsafa ya 4R, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zinakwenda kuyabadilisha mashirika haya na kuongeza kuwa na ufanisi na tija katika uwekezaji wa umma ili kuupaisha uchumi wa Tanzania.

Falsafa ya Dkt. Samia ya 4R, ambayo imeiweka Tanzania katika ramani ya mataifa yenye utulivu na mafanikio ya kiuchumi, sasa inaangazia jinsi mashirika ya umma (SOEs) yanavyoweza kuitumia falsafa hiyo kusimamia uwekezaji mkubwa wenye manufaa kwa nchi.

Ni kesho tarehe 27 Agosti, 2024, Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, anayaleta pamoja mashirika yote ya umma na yale ya binafsi, kukutana uso kwa uso na Mkuu wa Nchi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye siku ya Ahamisi, anatarajiwa kufungua Kikao kazi hicho kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.

“Ninatamani wateule wote wa Dkt. Samia wangekuwa wanamsaidia mama yetu kama huyu ndugu Msechu [akimaanisha Nehemiah Mchechu], alisema Kenaz Kulwa Obadiah, Mtaalamu wa sekta ya utalii jijini Arusha.

“Kwa mikakati hii, sasa mashirika hayatakuwa mizigo tena, liability [mzigo/deni] bali assets [mali],” aliongeza Bw. Obadiah.

Ni katika kikao hiki, mapinduzi makubwa katika ujenzi wa uchumi waTanzania kupitia mashirika yake, unakwenda kuasisiwa. Si siku nyingi, Mashirika haya yatavuka mipaka na kwenda kuleta hazina iliyositirika mbali, mithili ya China ilivyofanya hadi kuwa taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani.

Bw. Nehemiah Mchechu, Mwana mikakati mwenye vipaji, anayeratibu mashirika yote ya umma nchini, anasema, Kifungu cha 7 cha Sheria ya Mashirika ya Umma SURA 257, pamoja na mambo mengine, kimeelekeza Mashirika ya Umma kujiendesha kwa misingi thabiti ya kibiashara.

Mageuzi makubwa kwenye mashirika yamefanyika tangu Dkt. Samia alipomteua Bw. Mchechu kuwa Msajili wa Hazina. “Kumbe haya mashirikakuwa mzigo ni kukosa uongozi tu, sasa tunaona, mtu sahihi yuko ofisini, mashirika yanakuwa baraka na asset muhimu kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania,” anasema Rehema Sung’are, kutoka Monduli.

Katika Kikao kazi hicho cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa MashirikayaUmma cha mwaka jana, Dkt. Samia aliyataka Mashirika hayo kupanuauwekezaji wao hadi nje ya nchi ili kuongeza pato na faida kwa nchi.

China imeyatumia mashirika yake ya umma kuleta utajiri mkubwa nchini kwao. Nchini, sekta binafsi ikiongozwa na Benki za CRDB, Exim, METLna SSB (Bakhresa) tayari wako katika nchi kadhaa za Afrika.

Kikao hicho cha siku nne (4), kinatarajiwa kufungwa siku ya Ijumaa tarehe 30 Agosti, 2024. Kwa mujibu wa ratiba ya Kikao kazi hicho, pamoja na mambomengine, mashirika haya yatajadili namna ya kuitumia falsafa ya 4R kuleta ufanisi katika utendaji kazi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya Wenyeviti wa Bodi na Viongozi Wakuu wataasisi, inaangalia zaidi uwezekano wa mashirika haya ya umma, sio tu kujikita katika masoko ya ndani ya nchi, bali pia kutoka kwenda kuwekezanje ya nchi.

Naye Katibu wa Umoja wa Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, Bw. Abdul-Razak Badru, alisema maagizo waliyopewa na Rais Dkt. Samia, kupitia kwa Msajili wa Hazina, Bw. Mchechu, yalikuwa dira kwa utendaji kazi wao kwa kipindi cha mwaka mzima.

Bw. Badru ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), alisema maagizo hayo yalikuwa na mchango mkubwa katika kuleta matokeo mazuri.

“Yalitusaidia kuimarisha usimamizi, ufanisi, kupima matokeo ya utendaji, pamoja na kuongeza matumizi ya data na teknolojia, yaliyosaidia kuongeza tija katika majukumu yetu,” alisema. Bw. Abdul-Razak Badru Katibu CEOs Forum.

Katibu huyo wa CEOs Forum, alisema kwamba maelekezo waliyope wayalisaidia kuitafsiri falsafa ya 4R ya Rais Dkt. Samia katika utendaji waowakila siku na kwamba Wajumbe wake wamehamasika kupokea maelekezo mengine kwa ajili ya utekelezaji katika kikao cha mwaka huu.

Katika Mkutano huo ambao utahudhuliwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi yaRais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo, Rais Dkt. Samia atatoa tuzo kwa washindi mbalimbali.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kufanya mawasilisho yao kwenye mkutano huo, ni pamoja na Bw. Nehemiah Mchechu, Wawakilishi kutoka China, Singapore, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kutoka Shirika la Ndegela Ethiopia.

Chapisha Maoni

0 Maoni